Ezekieli 28:12
Ezekiel 28:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mwanadamu, mfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, nawe umwambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ulikuwa kipeo cha ukamilifu, ukiwa umejaa hekima na mkamilifu katika uzuri.
Ezekiel 28:12 in English
Ezekiel 28:12 · Berean Standard Bible
“Son of man, take up a lament for the king of Tyre and tell him that this is what the Lord GOD says: ‘You were the seal of perfection, full of wisdom and perfect in beauty.
Context
10Utakufa kifo cha wasiotahiriwa
kwa mkono wa wageni.
Kwa kuwa mimi nimenena, asema Bwana Mwenyezi.’ ” 11Neno la Bwana likanijia kusema: 12“Mwanadamu, mfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, nawe umwambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Ulikuwa kipeo cha ukamilifu,
ukiwa umejaa hekima
na mkamilifu katika uzuri. 13Ulikuwa ndani ya Edeni,
bustani ya Mungu;
kila kito cha thamani kilikupamba:
akiki nyekundu, yakuti manjano na zumaridi,
krisolitho, shohamu na yaspi,
yakuti samawi, almasi na zabarajadi.
Kuwekwa kwa hayo mapambo na kushikizwa kwake
kulifanywa kwa dhahabu;
siku ile ulipoumbwa yaliandaliwa tayari. 14Ulitiwa mafuta kuwa kerubi mlinzi,
kwa kuwa hivyo ndivyo nilivyokuweka wakfu.
Ulikuwa kwenye mlima mtakatifu wa Mungu;
ulitembea katikati ya vito vya moto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.