Ezekieli 27:11
Ezekiel 27:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu wa Arvadi na wa Heleki walikuwa juu ya kuta zako pande zote; watu wa Gamadi walikuwa kwenye minara yako. Walitundika ngao zao kuzizunguka kuta zako; wakaukamilisha uzuri wako.
Ezekiel 27:11 in English
Ezekiel 27:11 · Berean Standard Bible
Men of Arvad and Helech manned your walls all around, and the men of Gammad were in your towers. They hung their shields around your walls; they perfected your beauty.
Context
9Wazee wa Gebali* pamoja na mafundi stadi
walikuwa mafundi wako melini.
Meli zote za baharini na mabaharia wao
walikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako. 10“ ‘Watu wa Uajemi, Ludi na Putu
walikuwa askari katika jeshi lako.
Walitundika ngao zao na chapeo zao kwenye kuta zako,
wakileta fahari yako. 11Watu wa Arvadi na wa Heleki
walikuwa juu ya kuta zako pande zote;
watu wa Gamadi
walikuwa kwenye minara yako.
Walitundika ngao zao kuzizunguka kuta zako;
wakaukamilisha uzuri wako. 12“ ‘Tarshishi walifanya biashara nawe kwa sababu ya utajiri wako mkubwa wa bidhaa, walibadilisha fedha, chuma, bati na risasi kwa mali zako. 13“ ‘Uyunani, Tubali na Mesheki, walifanya biashara nawe, walibadilisha watumwa na vyombo vya shaba kwa bidhaa zako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.