Ezekieli 22:8
Ezekiel 22:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mmedharau vitu vyangu vitakatifu na kuzinajisi Sabato zangu.
Ezekiel 22:8 in English
Ezekiel 22:8 · Berean Standard Bible
You have despised My holy things and profaned My Sabbaths.
Context
6“ ‘Ona jinsi kila mkuu wa Israeli aliyeko ndani yako anavyotumia nguvu zake kumwaga damu. 7Ndani yako wamewadharau baba na mama, ndani yako wamewatendea wageni udhalimu na kuwaonea yatima na wajane. 8Mmedharau vitu vyangu vitakatifu na kuzinajisi Sabato zangu. 9Ndani yako wako watu wasingiziaji, watu walio tayari kumwaga damu, ndani yako wako wale wanaokula vyakula vilivyotolewa mahali pa ibada za miungu kwenye milima, na kutenda matendo ya uasherati. 10Ndani yako wako wale wanaovunjia heshima vitanda vya baba zao, ndani yako wamo wale wanaowatendea wanawake jeuri wakiwa katika hedhi, wakati wakiwa si safi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.