Native Bible

Ezekiel 22:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndani yako wamewadharau baba na mama, ndani yako wamewatendea wageni udhalimu na kuwaonea yatima na wajane.

Ezekiel 22:7 in English

Ezekiel 22:7 · Berean Standard Bible

Father and mother are treated with contempt. Within your walls the foreign resident is exploited, the fatherless and the widow are oppressed.

Context

5Wale walio karibu na wale walio mbali watakudhihaki, Ewe mji wenye sifa mbaya, uliyejaa ghasia. 6“ ‘Ona jinsi kila mkuu wa Israeli aliyeko ndani yako anavyotumia nguvu zake kumwaga damu. 7Ndani yako wamewadharau baba na mama, ndani yako wamewatendea wageni udhalimu na kuwaonea yatima na wajane. 8Mmedharau vitu vyangu vitakatifu na kuzinajisi Sabato zangu. 9Ndani yako wako watu wasingiziaji, watu walio tayari kumwaga damu, ndani yako wako wale wanaokula vyakula vilivyotolewa mahali pa ibada za miungu kwenye milima, na kutenda matendo ya uasherati.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.