Ezekieli 18:17
Ezekiel 18:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Huuzuia mkono wake usitende dhambi, hakopeshi kwa riba wala hajipatii faida ya ziada. Huzishika amri zangu na kuzifuata sheria zangu. Hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake; hakika ataishi.
Ezekiel 18:17 in English
Ezekiel 18:17 · Berean Standard Bible
He withholds his hand from harming the poor * and takes no interest or usury. He keeps My ordinances and follows My statutes. Such a man will not die for his father’s iniquity. He will surely live.
Context
15“Hakula katika mahali pa ibada za miungu
kwenye milima,
wala hainulii macho sanamu
za nyumba ya Israeli.
Hakumtia unajisi
mke wa jirani yake. 16Hakumwonea mtu yeyote
wala hakutaka rehani kwa ajili ya mkopo.
Hanyangʼanyi,
bali huwapa wenye njaa chakula chake
na huwapa nguo walio uchi. 17Huuzuia mkono wake usitende dhambi,
hakopeshi kwa riba
wala hajipatii faida ya ziada.
Huzishika amri zangu
na kuzifuata sheria zangu.
Hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake; hakika ataishi. 18Lakini baba yake atakufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe, kwa sababu alitoza bei isiyo halali kwa nguvu, akamnyangʼanya ndugu yake na kufanya yaliyo mabaya miongoni mwa watu wake. 19“Lakini mnauliza, ‘Kwa nini mwana asiadhibiwe kwa uovu wa baba yake?’ Kwa vile mwana ametenda yaliyo haki na sawa na amekuwa mwangalifu kuzishika amri zangu zote, hakika ataishi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.