Ezekieli 18:12
Ezekiel 18:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Huwaonea maskini na wahitaji. Hunyangʼanyana. Harudishi kile kilichowekwa rehani kwake. Huziinulia sanamu macho. Hufanya mambo ya machukizo.
Ezekiel 18:12 in English
Ezekiel 18:12 · Berean Standard Bible
He oppresses the poor and needy; he commits robbery and does not restore a pledge. He lifts his eyes to idols; he commits abominations.
Context
10“Aweza kuwa ana mwana jeuri, amwagaye damu au atendaye mojawapo ya mambo haya 11(ingawa baba yake hakufanya mojawapo ya haya):
“Hula katika mahali pa ibada za miungu kwenye milima.
Humtia unajisi mke wa jirani yake. 12Huwaonea maskini na wahitaji.
Hunyangʼanyana.
Harudishi kile kilichowekwa rehani kwake.
Huziinulia sanamu macho.
Hufanya mambo ya machukizo. 13Hukopesha kwa riba na kutafuta faida ya ziada.
Je, mtu wa namna hii ataishi? Hapana, hataishi! Kwa sababu amefanya mambo haya yote ya machukizo, hakika atauawa na damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. 14“Lakini yawezekana mwana huyo ana mwana aonaye dhambi hizi zote anazofanya baba yake, naye ingawa anaziona, yeye hafanyi mabaya kama haya:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.