Ezekieli 16:9
Ezekiel 16:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“ ‘Nilikuogesha kwa maji, nikakuosha ile damu na kukupaka mafuta.
Ezekiel 16:9 in English
Ezekiel 16:9 · Berean Standard Bible
Then I bathed you with water, rinsed off your blood, and anointed you with oil.
Context
7Nilikufanya uote kama mmea wa shambani. Ukakua na kuongezeka sana, ukawa kito cha thamani kuliko vyote. Matiti yako yakatokeza na nywele zako zikaota, wewe uliyekuwa uchi na bila kitu chochote. 8“ ‘Baadaye nikapita karibu nawe, nilipokutazama na kukuona kuwa umefikia umri wa kupendwa, nililitandaza vazi langu juu yako na kuufunika uchi wako. Nikakuapia na kuingia kwenye Agano na wewe, asema Bwana Mwenyezi, nawe ukawa wangu. 9“ ‘Nilikuogesha kwa maji, nikakuosha ile damu na kukupaka mafuta. 10Nikakuvika vazi lililotariziwa na kukuvalisha viatu vya kamba vya ngozi. Nikakuvika nguo za kitani safi na kukufunika kwa mavazi ya thamani kubwa. 11Nikakupamba kwa vito: nikakuvika bangili mikononi mwako na mkufu shingoni mwako,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.