Ezekieli 16:10
Ezekiel 16:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nikakuvika vazi lililotariziwa na kukuvalisha viatu vya kamba vya ngozi. Nikakuvika nguo za kitani safi na kukufunika kwa mavazi ya thamani kubwa.
Ezekiel 16:10 in English
Ezekiel 16:10 · Berean Standard Bible
I clothed you in embroidered cloth and gave you sandals of fine leather. I wrapped you in fine linen and covered you with silk.
Context
8“ ‘Baadaye nikapita karibu nawe, nilipokutazama na kukuona kuwa umefikia umri wa kupendwa, nililitandaza vazi langu juu yako na kuufunika uchi wako. Nikakuapia na kuingia kwenye Agano na wewe, asema Bwana Mwenyezi, nawe ukawa wangu. 9“ ‘Nilikuogesha kwa maji, nikakuosha ile damu na kukupaka mafuta. 10Nikakuvika vazi lililotariziwa na kukuvalisha viatu vya kamba vya ngozi. Nikakuvika nguo za kitani safi na kukufunika kwa mavazi ya thamani kubwa. 11Nikakupamba kwa vito: nikakuvika bangili mikononi mwako na mkufu shingoni mwako, 12nikaweka hazama puani mwako, vipuli masikioni mwako na taji nzuri sana kichwani mwako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.