Native Bible

Ezekiel 16:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nikakupamba kwa vito: nikakuvika bangili mikononi mwako na mkufu shingoni mwako,

Ezekiel 16:11 in English

Ezekiel 16:11 · Berean Standard Bible

I adorned you with jewelry, and I put bracelets on your wrists and a chain around your neck.

Context

9“ ‘Nilikuogesha kwa maji, nikakuosha ile damu na kukupaka mafuta. 10Nikakuvika vazi lililotariziwa na kukuvalisha viatu vya kamba vya ngozi. Nikakuvika nguo za kitani safi na kukufunika kwa mavazi ya thamani kubwa. 11Nikakupamba kwa vito: nikakuvika bangili mikononi mwako na mkufu shingoni mwako, 12nikaweka hazama puani mwako, vipuli masikioni mwako na taji nzuri sana kichwani mwako. 13Kwa hiyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha, nguo zako zilikuwa za kitani safi, hariri na nguo iliyokuwa imetariziwa. Chakula chako kilikuwa unga laini, asali na mafuta ya zeituni. Ukawa mzuri sana ukainuka kuwa malkia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.