Native Bible

Ezekiel 13:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Manabii wako, ee Israeli, ni kama mbweha katikati ya magofu.

Ezekiel 13:4 in English

Ezekiel 13:4 · Berean Standard Bible

Your prophets, O Israel, are like foxes among the ruins.

Context

2“Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wa Israeli wanaotabiri sasa. Waambie hao ambao hutabiri kutokana na mawazo yao wenyewe: ‘Sikia neno la Bwana! 3Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ole wao manabii wapumbavu wafuatao roho yao wenyewe na wala hawajaona chochote! 4Manabii wako, ee Israeli, ni kama mbweha katikati ya magofu. 5Hamjakwea kwenda kuziba mahali palipobomoka katika ukuta ili kuukarabati kwa ajili ya nyumba ya Israeli, ili kwamba isimame imara kwenye vita katika siku ya Bwana. 6Maono yao ni ya uongo na ubashiri wao ni wa udanganyifu. Wao husema, “Bwana amesema,” wakati Bwana hakuwatuma, bado wakitarajia maneno yao kutimizwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.