Ezekieli 13:3
Ezekiel 13:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ole wao manabii wapumbavu wafuatao roho yao wenyewe na wala hawajaona chochote!
Ezekiel 13:3 in English
Ezekiel 13:3 · Berean Standard Bible
This is what the Lord GOD says: Woe to the foolish prophets who follow their own spirit, yet have seen nothing.
Context
1Neno la Bwana likanijia kusema: 2“Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wa Israeli wanaotabiri sasa. Waambie hao ambao hutabiri kutokana na mawazo yao wenyewe: ‘Sikia neno la Bwana! 3Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ole wao manabii wapumbavu wafuatao roho yao wenyewe na wala hawajaona chochote! 4Manabii wako, ee Israeli, ni kama mbweha katikati ya magofu. 5Hamjakwea kwenda kuziba mahali palipobomoka katika ukuta ili kuukarabati kwa ajili ya nyumba ya Israeli, ili kwamba isimame imara kwenye vita katika siku ya Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.