Kutoka 40:22
Exodus 40:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mose akaweka meza ndani ya Hema la Kukutania, upande wa kaskazini ya Maskani ya Mungu nje ya pazia
Exodus 40:22 in English
Exodus 40:22 · Berean Standard Bible
Moses placed the table in the Tent of Meeting on the north side of the tabernacle, outside the veil.
Context
20Akachukua ule Ushuhuda na kuuweka ndani ya Sanduku la Agano, akaweka ile mipiko ya kubebea hilo Sanduku na kuweka kiti cha rehema juu yake. 21Kisha Mose akalileta Sanduku ndani ya Maskani ya Mungu, akatundika pazia ili kulifunika Sanduku la Ushuhuda, kama Bwana alivyomwagiza. 22Mose akaweka meza ndani ya Hema la Kukutania, upande wa kaskazini ya Maskani ya Mungu nje ya pazia 23na kupanga mikate juu yake mbele za Bwana, kama Bwana alivyomwagiza. 24Akaweka kinara cha taa ndani ya Hema la Kukutania mkabala na meza upande wa kusini mwa Maskani ya Mungu
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.