Native Bible

Exodus 39:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

safu ya pili ilikuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi;

Exodus 39:11 in English

Exodus 39:11 · Berean Standard Bible

the second row had a turquoise, a sapphire, and a diamond;

Context

9Kifuko hicho kilikuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja* na upana wa shibiri moja, nacho kilikunjwa mara mbili. 10Kifuko hicho kilipambwa kwa safu nne za vito vya thamani. Safu ya kwanza ilikuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; 11safu ya pili ilikuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; 12safu ya tatu ilikuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; 13katika safu ya nne ilikuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Vito hivyo vilitiwa kwenye vijalizo vya dhahabu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.