Kutoka 38:10
Exodus 38:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
Exodus 38:10 in English
Exodus 38:10 · Berean Standard Bible
with twenty posts and twenty bronze bases, and with silver hooks and bands on the posts.
Context
8Akatengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kutoka kwa vioo vya shaba vilivyotolewa na wanawake waliohudumu pale ingilio la Hema la Kukutania. 9Kisha akatengeneza ua. Upande wa kusini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja,* na ulikuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, 10pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 11Upande wa kaskazini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 12Upande wa mwisho wa magharibi ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini* na ulikuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.