Native Bible

Exodus 33:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana akamwambia Mose, “Nitakufanyia jambo lile uliloomba, kwa sababu ninapendezwa nawe, nami ninakujua kwa jina lako.”

Exodus 33:17 in English

Exodus 33:17 · Berean Standard Bible

So the LORD said to Moses, “I will do this very thing you have asked, for you have found favor in My sight, and I know you by name.”

Context

15Kisha Mose akamwambia, “Kama Uso wako hauendi pamoja nasi, usituondoe hapa. 16Mtu yeyote atajuaje kuwa mimi pamoja na watu wako tumepata kibali mbele zako, usipokwenda pamoja nasi? Ni nini kingine kitakachoweza kututofautisha mimi na watu wako miongoni mwa watu wengine wote walio katika uso wa dunia?” 17Bwana akamwambia Mose, “Nitakufanyia jambo lile uliloomba, kwa sababu ninapendezwa nawe, nami ninakujua kwa jina lako.” 18Kisha Mose akasema, “Basi nionyeshe utukufu wako.” 19Ndipo Bwana akasema, “Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza Jina langu, Bwana, mbele ya uso wako. Nitamrehemu yeye nimrehemuye, na pia nitamhurumia yeye nimhurumiaye.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.