Native Bible

Exodus 33:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana akajibu, “Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.”

Exodus 33:14 in English

Exodus 33:14 · Berean Standard Bible

And the LORD answered, “My Presence will go with you, and I will give you rest.”

Context

12Mose akamwambia Bwana, “Umekuwa ukiniambia, ‘Ongoza watu hawa,’ lakini hujanifahamisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Umesema, ‘Ninakujua wewe kwa jina lako, nawe umepata kibali mbele zangu.’ 13Ikiwa umependezwa nami, nifundishe njia zako ili nipate kukujua, nami nizidi kupata kibali mbele zako. Kumbuka kuwa taifa hili ni watu wako.” 14Bwana akajibu, “Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.” 15Kisha Mose akamwambia, “Kama Uso wako hauendi pamoja nasi, usituondoe hapa. 16Mtu yeyote atajuaje kuwa mimi pamoja na watu wako tumepata kibali mbele zako, usipokwenda pamoja nasi? Ni nini kingine kitakachoweza kututofautisha mimi na watu wako miongoni mwa watu wengine wote walio katika uso wa dunia?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.