Kutoka 30:19
Exodus 30:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Aroni na wanawe watanawa mikono na miguu yao kwa maji yatokayo katika hilo sinia.
Exodus 30:19 in English
Exodus 30:19 · Berean Standard Bible
with which Aaron and his sons are to wash their hands and feet.
Context
17Kisha Bwana akamwambia Mose, 18“Tengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kwa ajili ya kunawia. Liweke kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, kisha uweke maji ndani yake. 19Aroni na wanawe watanawa mikono na miguu yao kwa maji yatokayo katika hilo sinia. 20Wakati wowote wanapoingia katika Hema la Kukutania, watanawa kwa maji ili kwamba wasije wakafa. Pia, wanapokaribia madhabahu ili kuhudumu kwa kuleta sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto, 21watanawa mikono na miguu yao ili kwamba wasije wakafa. Hii itakuwa ni amri ya kudumu kwa ajili ya Aroni na wazao wake kwa vizazi vijavyo.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.