Native Bible

Exodus 29:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Kwa kawaida hiki ndicho utakachotoa juu ya madhabahu kila siku: wana-kondoo wawili wenye umri wa mwaka mmoja.

Exodus 29:38 in English

Exodus 29:38 · Berean Standard Bible

This is what you are to offer regularly on the altar, each day: two lambs that are a year old.

Context

36Utatoa dhabihu ya fahali kila siku kuwa sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho. Takasa madhabahu kwa kufanya upatanisho kwa ajili yake, nayo uitie mafuta na kuiweka wakfu. 37Kwa muda wa siku saba fanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu na kuiweka wakfu. Ndipo madhabahu itakuwa takatifu sana na chochote kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu. 38“Kwa kawaida hiki ndicho utakachotoa juu ya madhabahu kila siku: wana-kondoo wawili wenye umri wa mwaka mmoja. 39Utamtoa mmoja asubuhi na huyo mwingine jioni. 40Pamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa moja* ya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hini* ya mafuta yaliyokamuliwa, pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.