Native Bible

Exodus 29:40 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Pamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa moja* ya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hini* ya mafuta yaliyokamuliwa, pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji.

Exodus 29:40 in English

Exodus 29:40 · Berean Standard Bible

With the first lamb offer a tenth of an ephah of fine flour,* mixed with a quarter hin of oil from pressed olives,* and a drink offering of a quarter hin of wine.

Context

38“Kwa kawaida hiki ndicho utakachotoa juu ya madhabahu kila siku: wana-kondoo wawili wenye umri wa mwaka mmoja. 39Utamtoa mmoja asubuhi na huyo mwingine jioni. 40Pamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa moja* ya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hini* ya mafuta yaliyokamuliwa, pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji. 41Huyo mwana-kondoo mwingine mtoe dhabihu wakati wa machweo pamoja na sadaka za unga na za kinywaji kama vile ulivyofanya asubuhi, kuwa harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. 42“Kwa vizazi vijavyo itakuwa kawaida kutoa sadaka hii ya kuteketezwa kila mara kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za Bwana. Hapo ndipo nitakapokutana na ninyi na kusema nanyi,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.