Kutoka 29:11
Exodus 29:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mchinje huyo fahali mbele za Bwana kwenye mlango wa Hema la Kukutania.
Exodus 29:11 in English
Exodus 29:11 · Berean Standard Bible
And you shall slaughter the bull before the LORD at the entrance to the Tent of Meeting.
Context
9pia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Aroni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamweka wakfu Aroni na wanawe. 10“Mlete yule fahali mbele ya Hema la Kukutania, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake. 11Mchinje huyo fahali mbele za Bwana kwenye mlango wa Hema la Kukutania. 12Chukua sehemu ya damu ya huyo fahali na kuipaka kwenye pembe za hayo madhabahu kwa kidole chako, na damu iliyobaki uimwage sehemu ya chini ya madhabahu. 13Kisha chukua mafuta yote ya huyo mnyama ya sehemu za ndani, yale yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, uviteketeze juu ya madhabahu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.