Native Bible

Exodus 28:42 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Watengenezee nguo za ndani za kitani zitakazofunika mwili, kutoka kiunoni hadi mapajani.

Exodus 28:42 in English

Exodus 28:42 · Berean Standard Bible

Make linen undergarments to cover their bare flesh, extending from waist to thigh.

Context

40Watengenezee wana wa Aroni makoti, mishipi na kofia, ili kuwapa ukuu na heshima. 41Baada ya kumvika Aroni ndugu yako pamoja na wanawe nguo hizi, watie mafuta na kuwabariki. Waweke wakfu ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. 42“Watengenezee nguo za ndani za kitani zitakazofunika mwili, kutoka kiunoni hadi mapajani. 43Aroni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma katika Mahali Patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa. “Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Aroni na vizazi vyake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.