Kutoka 28:40
Exodus 28:40 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watengenezee wana wa Aroni makoti, mishipi na kofia, ili kuwapa ukuu na heshima.
Exodus 28:40 in English
Exodus 28:40 · Berean Standard Bible
Make tunics, sashes, and headbands for Aaron’s sons, to give them glory and splendor.
Context
38Aroni alivae bamba hilo kwenye paji la uso wake, naye atachukua hatia kuhusu sadaka takatifu za Waisraeli wanazoweka wakfu, sadaka za aina yoyote. Litakuwa kwenye paji la uso wa Aroni daima ili zikubalike kwa Bwana. 39“Fuma koti la kitani safi na ufanye kilemba cha kitani safi. Mshipi uwe ni kazi ya mtarizi. 40Watengenezee wana wa Aroni makoti, mishipi na kofia, ili kuwapa ukuu na heshima. 41Baada ya kumvika Aroni ndugu yako pamoja na wanawe nguo hizi, watie mafuta na kuwabariki. Waweke wakfu ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. 42“Watengenezee nguo za ndani za kitani zitakazofunika mwili, kutoka kiunoni hadi mapajani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.