Native Bible

Exodus 27:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

Exodus 27:10 in English

Exodus 27:10 · Berean Standard Bible

with twenty posts and twenty bronze bases, and silver hooks and bands on the posts.

Context

8Tengeneza madhabahu yawe na uvungu ndani yake ukitumia mbao. Utaitengeneza sawasawa na vile ulivyoonyeshwa mlimani. 9“Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja,* na utakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, 10pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 11Upande wa kaskazini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. 12“Upande wa magharibi wa ua utakuwa na upana wa dhiraa hamsini,* nao utakuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.