Native Bible

Exodus 27:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tengeneza madhabahu yawe na uvungu ndani yake ukitumia mbao. Utaitengeneza sawasawa na vile ulivyoonyeshwa mlimani.

Exodus 27:8 in English

Exodus 27:8 · Berean Standard Bible

Construct the altar with boards so that it is hollow. It is to be made just as you were shown on the mountain.

Context

6Tengeneza mipiko ya mti wa mshita kwa ajili ya madhabahu, na uifunike kwa shaba. 7Hiyo mipiko itaingizwa kwenye zile pete ili iwe pande mbili za madhabahu inapobebwa. 8Tengeneza madhabahu yawe na uvungu ndani yake ukitumia mbao. Utaitengeneza sawasawa na vile ulivyoonyeshwa mlimani. 9“Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja,* na utakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, 10pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.