Native Bible

Exodus 26:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, na ufanye vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho.

Exodus 26:4 in English

Exodus 26:4 · Berean Standard Bible

Make loops of blue material on the edge of the end curtain in the first set, and do the same for the end curtain in the second set.

Context

2Mapazia yote yatatoshana kwa ukubwa: kila moja litakuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane,* na upana wa dhiraa nne* 3Unganisha mapazia matano pamoja; fanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. 4Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, na ufanye vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho. 5Fanya vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, nazo vitanzi vyote vielekeane. 6Kisha tengeneza vifungo hamsini vya dhahabu ili vitumike kufunga na kuunganisha mapazia pamoja kufanya Hema liwe kitu kimoja.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.