Kutoka 26:3
Exodus 26:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Unganisha mapazia matano pamoja; fanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano.
Exodus 26:3 in English
Exodus 26:3 · Berean Standard Bible
Five of the curtains are to be joined together, and the other five joined as well.
Context
1“Tengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi atatarizi makerubi kwenye mapazia hayo. 2Mapazia yote yatatoshana kwa ukubwa: kila moja litakuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane,* na upana wa dhiraa nne* 3Unganisha mapazia matano pamoja; fanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. 4Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, na ufanye vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho. 5Fanya vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, nazo vitanzi vyote vielekeane.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.