Native Bible

Exodus 21:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Kama mtu akiacha shimo wazi, ama akachimba shimo kisha asilifukie, na ngʼombe au punda akatumbukia ndani yake,

Exodus 21:33 in English

Exodus 21:33 · Berean Standard Bible

If a man opens or digs a pit and fails to cover it, and an ox or a donkey falls into it,

Context

31Sheria hii pia itatumika ikiwa fahali atampiga kwa pembe mwana au binti. 32Ikiwa fahali atampiga mtumwa wa kike au wa kiume, mwenye fahali atalipa shekeli thelathini* za fedha kwa bwana mwenye mtumwa, na fahali ni lazima auawe kwa mawe. 33“Kama mtu akiacha shimo wazi, ama akachimba shimo kisha asilifukie, na ngʼombe au punda akatumbukia ndani yake, 34mwenye shimo ni lazima alipe hasara iliyotokea; ni lazima amlipe mwenye mnyama. Mnyama aliyekufa atakuwa wake. 35“Kama fahali wa mtu fulani atamuumiza fahali wa mtu mwingine na akafa, watamuuza yule aliye hai na wagawane sawa fedha pamoja na mnyama aliyekufa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.