Native Bible

Exodus 21:30 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini ikiwa malipo yatatakiwa kwake, basi anaweza kulipa kinachodaiwa ili kuukomboa uhai wake.

Exodus 21:30 in English

Exodus 21:30 · Berean Standard Bible

If payment is demanded of him instead, he may redeem his life by paying the full amount demanded of him.

Context

28“Kama fahali akimuua mwanaume au mwanamke kwa kumpiga kwa pembe, fahali huyo ni lazima auawe kwa kupigwa mawe, na nyama yake haitaliwa. Lakini mwenye fahali huyo hatawajibika. 29Lakini hata hivyo, ikiwa huyo fahali amekuwa na tabia ya kupiga kwa pembe, na mwenyewe ameonywa na hakutaka kumfungia naye akamuua mwanaume au mwanamke, huyo fahali ni lazima auawe kwa mawe na mwenye fahali pia auawe. 30Lakini ikiwa malipo yatatakiwa kwake, basi anaweza kulipa kinachodaiwa ili kuukomboa uhai wake. 31Sheria hii pia itatumika ikiwa fahali atampiga kwa pembe mwana au binti. 32Ikiwa fahali atampiga mtumwa wa kike au wa kiume, mwenye fahali atalipa shekeli thelathini* za fedha kwa bwana mwenye mtumwa, na fahali ni lazima auawe kwa mawe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.