Kutoka 20:8
Exodus 20:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ikumbuke siku ya Sabato, uitakase.
Exodus 20:8 in English
Exodus 20:8 · Berean Standard Bible
Remember the Sabbath day by keeping it holy.
Context
6lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu. 7Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure. 8Ikumbuke siku ya Sabato, uitakase. 9Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote, 10lakini siku ya saba ni Sabato kwa Bwana Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike, wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.