Native Bible

Exodus 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Naili.

Exodus 2:3 in English

Exodus 2:3 · Berean Standard Bible

But when she could no longer hide him, she got him a papyrus basket * and coated it with tar and pitch. Then she placed the child in the basket and set it among the reeds along the bank of the Nile.

Context

1Basi mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaoa mwanamke Mlawi, 2naye mwanamke huyo akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Alipoona mtoto huyo ni mzuri, akamficha kwa miezi mitatu. 3Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Naili. 4Dada ya huyo mtoto akasimama mbali ili kuona kitakachompata mtoto. 5Ndipo binti Farao akateremka mtoni Naili kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti mfalme akaona kisafina katikati ya manyasi, akamtuma mmoja wa watumwa wake wa kike kukichukua.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.