Kutoka 2:4
Exodus 2:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Dada ya huyo mtoto akasimama mbali ili kuona kitakachompata mtoto.
Exodus 2:4 in English
Exodus 2:4 · Berean Standard Bible
And his sister stood at a distance to see what would happen to him.
Context
2naye mwanamke huyo akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Alipoona mtoto huyo ni mzuri, akamficha kwa miezi mitatu. 3Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Naili. 4Dada ya huyo mtoto akasimama mbali ili kuona kitakachompata mtoto. 5Ndipo binti Farao akateremka mtoni Naili kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti mfalme akaona kisafina katikati ya manyasi, akamtuma mmoja wa watumwa wake wa kike kukichukua. 6Alifungua kisafina akaona mtoto ndani yake. Mtoto alikuwa akilia, akamhurumia. Akasema, “Huyu ni mmoja wa watoto wa Kiebrania.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.