Native Bible

Exodus 2:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaoa mwanamke Mlawi,

Exodus 2:1 in English

Exodus 2:1 · Berean Standard Bible

Now a man of the house of Levi married a daughter of Levi,

Context

1Basi mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaoa mwanamke Mlawi, 2naye mwanamke huyo akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Alipoona mtoto huyo ni mzuri, akamficha kwa miezi mitatu. 3Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Naili.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.