Kutoka 13:10
Exodus 13:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni lazima uishike amri hii kwa wakati uliopangwa mwaka baada ya mwaka.
Exodus 13:10 in English
Exodus 13:10 · Berean Standard Bible
Therefore you shall keep this statute at the appointed time year after year.
Context
8Siku ile utamwambia mwanao, ‘Nafanya hivi kwa sababu ya jambo ambalo Bwana alinitendea nilipotoka katika nchi ya Misri.’ 9Adhimisho hili, litakuwa kama alama kwenye mkono wako na ukumbusho katika paji lako la uso, kwamba sheria ya Bwana inapaswa iwe kinywani mwako. Kwa kuwa Bwana alikutoa katika nchi ya Misri kwa mkono wake wenye nguvu. 10Ni lazima uishike amri hii kwa wakati uliopangwa mwaka baada ya mwaka. 11“Baada ya Bwana kukuingiza katika nchi ya Wakanaani na kukupa nchi hiyo, kama alivyokuahidi kwa kiapo na kwa baba zako, 12inakupasa kumtolea Bwana mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo. Wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa mifugo yako ni mali ya Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.