Kutoka 12:41
Exodus 12:41 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ilikuwa ni siku ya mwisho ya hiyo miaka 430, vikosi vyote vya Bwana vilipokuwa vimeondoka Misri.
Exodus 12:41 in English
Exodus 12:41 · Berean Standard Bible
At the end of the 430 years, to the very day, all the LORD’s divisions went out of the land of Egypt.
Context
39Wakatengeneza maandazi yasiyotiwa chachu kwa ule unga uliokandwa waliokuwa wameutoa Misri, donge hilo la unga halikuwa limetiwa chachu, kwa kuwa walikuwa wameondolewa Misri kwa haraka nao hawakuwa na muda wa kuandaa chakula chao. 40Waisraeli walikuwa wameishi Misri kwa muda wa miaka 430. 41Ilikuwa ni siku ya mwisho ya hiyo miaka 430, vikosi vyote vya Bwana vilipokuwa vimeondoka Misri. 42Kwa sababu Bwana aliutenga usiku ule ili kuwatoa Waisraeli katika nchi ya Misri, katika usiku huu Waisraeli wote wanapaswa kuadhimisha kwa kukesha ili kumheshimu Bwana katika vizazi vijavyo. 43Bwana akamwambia Mose na Aroni, “Haya ndiyo masharti kwa ajili ya Pasaka:
“Mgeni hataruhusiwa kula Pasaka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.