Esta 3:11
Esther 3:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mfalme akamwambia Hamani, “Baki na fedha yako na uwatendee hao watu utakavyo.”
Esther 3:11 in English
Esther 3:11 · Berean Standard Bible
“Keep your money,” said the king to Haman. “These people are given to you to do with them as you please.”
Context
9Kama inampendeza mfalme, itolewe amri kuwaangamiza, nami nitaweka talanta 10,000* za fedha katika hazina ya mfalme kwa ajili ya watu watakaoshughulikia jambo hili.” 10Basi mfalme alichukua pete yake ya muhuri kutoka kwenye kidole chake na kumpa Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, adui wa Wayahudi. 11Mfalme akamwambia Hamani, “Baki na fedha yako na uwatendee hao watu utakavyo.” 12Kisha siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza waandishi wa mfalme waliitwa. Wakaandika barua kwa kila jimbo na katika kila lugha ya watu kama agizo la Hamani lilivyotoka kwa mfalme, kwa watawala wa majimbo mbalimbali, na wakuu wa watu mbalimbali. Hizi ziliandikwa kwa jina la Mfalme Ahasuero mwenyewe na kutiwa muhuri wa pete yake mwenyewe. 13Barua zilipelekwa na tarishi katika majimbo yote ya mfalme zikiwa na amri ya kuharibu, kuua na kuangamiza Wayahudi wote, wadogo kwa wakubwa, wanawake na watoto wadogo, siku moja, yaani siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari, na pia kuteka nyara vitu vyao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.