Esta 3:9
Esther 3:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama inampendeza mfalme, itolewe amri kuwaangamiza, nami nitaweka talanta 10,000* za fedha katika hazina ya mfalme kwa ajili ya watu watakaoshughulikia jambo hili.”
Esther 3:9 in English
Esther 3:9 · Berean Standard Bible
If it pleases the king, let a decree be issued to destroy them, and I will deposit ten thousand talents of silver * into the royal treasury to pay those who carry it out.”
Context
7Katika mwaka wa kumi na mbili wa utawala wa Mfalme Ahasuero, katika mwezi wa kwanza uitwao Nisani, walipiga puri (yaani kura) mbele ya Hamani ili kuchagua siku na mwezi. Kura ikaangukia kwenye mwezi wa kumi na mbili, yaani Adari. 8Kisha Hamani akamwambia Mfalme Ahasuero, “Wako watu fulani wameenea na kutawanyika miongoni mwa watu katika majimbo yote ya ufalme wako, ambao desturi zao ni tofauti na zile za watu wengine wote, nao hawatii sheria za mfalme. Haifai mfalme kuwavumilia watu hawa. 9Kama inampendeza mfalme, itolewe amri kuwaangamiza, nami nitaweka talanta 10,000* za fedha katika hazina ya mfalme kwa ajili ya watu watakaoshughulikia jambo hili.” 10Basi mfalme alichukua pete yake ya muhuri kutoka kwenye kidole chake na kumpa Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, adui wa Wayahudi. 11Mfalme akamwambia Hamani, “Baki na fedha yako na uwatendee hao watu utakavyo.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.