Native Bible

Ephesians 5:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake

Ephesians 5:25 in English

Ephesians 5:25 · Berean Standard Bible

Husbands, love your wives, just as Christ loved the church and gave Himself up for her

Context

23Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha Kanisa, ambalo ni mwili wake, naye Kristo ni Mwokozi wake. 24Basi, kama vile Kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo. 25Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama vile Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa kwa ajili yake 26kusudi alifanye takatifu, akilitakasa kwa kuliosha kwa maji katika Neno lake, 27apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lolote, bali takatifu na lisilo na hatia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.