Waefeso 5:2
Ephesians 5:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
mkiishi maisha ya upendo, kama vile Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu.
Ephesians 5:2 in English
Ephesians 5:2 · Berean Standard Bible
and walk in love, just as Christ loved us * and gave Himself up for us as a fragrant sacrificial offering to God.
Context
1Kwa hiyo, mfuateni Mungu kama watoto wapendwao, 2mkiishi maisha ya upendo, kama vile Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu. 3Lakini uasherati, usitajwe miongoni mwenu, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu. 4Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.