Mhubiri 8:6
Ecclesiastes 8:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana kuna wakati muafaka na utaratibu wa kila jambo, ingawa huzuni ya mwanadamu huwa nzito juu yake.
Ecclesiastes 8:6 in English
Ecclesiastes 8:6 · Berean Standard Bible
For there is a right time and procedure to every purpose, though a man’s misery weighs heavily upon him.
Context
4Kwa kuwa neno la mfalme ndilo lenye mamlaka ya mwisho, nani awezaye kumwambia, “Je, wewe unafanya nini?” 5Yeyote anayetii agizo lake hatadhurika,
moyo wa hekima utajua wakati muafaka
na jinsi ya kutenda. 6Kwa maana kuna wakati muafaka
na utaratibu wa kila jambo,
ingawa huzuni ya mwanadamu
huwa nzito juu yake. 7Kwa vile hakuna mtu ajuaye siku zijazo,
ni nani awezaye kumwambia linalokuja? 8Hakuna mwanadamu
awezaye kushikilia roho yake asife,
wala hakuna mwenye uwezo
juu ya siku ya kufa kwake.
Kama vile hakuna yeyote arudishwaye nyuma wakati wa vita,
kadhalika uovu hautawaweka huru wale wautendao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.