Mhubiri 7:2
Ecclesiastes 7:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Afadhali kwenda kwenye nyumba ya msiba kuliko kwenda kwenye nyumba ya karamu, kwa kuwa kifo ni hatima ya kila mwanadamu, imewapasa walio hai kuliweka hili mioyoni mwao.
Ecclesiastes 7:2 in English
Ecclesiastes 7:2 · Berean Standard Bible
It is better to enter a house of mourning than a house of feasting, since death is the end of every man, and the living should take this to heart.
Context
1Afadhali sifa nzuri kuliko manukato safi,
nayo siku ya kufa kuliko ya kuzaliwa. 2Afadhali kwenda kwenye nyumba ya msiba
kuliko kwenda kwenye nyumba ya karamu,
kwa kuwa kifo ni hatima ya kila mwanadamu,
imewapasa walio hai kuliweka hili mioyoni mwao. 3Huzuni ni afadhali kuliko kicheko,
kwa sababu uso wenye huzuni wafaa kwa moyo. 4Moyo wa wenye hekima uko katika nyumba ya msiba,
lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya anasa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.