Native Bible

Ecclesiastes 6:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kuzaliwa kwake hakuna maana, huondokea gizani na gizani jina lake hufunikwa.

Ecclesiastes 6:4 in English

Ecclesiastes 6:4 · Berean Standard Bible

For a stillborn child enters in futility and departs in darkness, and his name is shrouded in obscurity.

Context

2Mungu humpa mwanadamu utajiri, mali na heshima, hivyo hakukosa chochote moyo wake unachokitamani. Lakini Mungu hamwezeshi kuvifurahia, badala yake mgeni ndiye anayevifurahia. Hili ni ubatili, ni ubaya unaosikitisha. 3Mtu anaweza kuwa na watoto mia moja naye akaishi miaka mingi, lakini haidhuru kuwa ataishi muda mrefu kiasi gani, kama hawezi kufurahia mafanikio yake na kwamba hapati mazishi ya heshima, ninasema afadhali mtoto aliyezaliwa akiwa amekufa kuliko yeye. 4Kuzaliwa kwake hakuna maana, huondokea gizani na gizani jina lake hufunikwa. 5Ingawa hakuwahi kuliona jua wala kujua kitu chochote, yeye ana pumziko zaidi kuliko mtu huyo, 6Hata kama huyo mtu ataishi miaka elfu mara mbili na zaidi, lakini akashindwa kufurahia mafanikio yake, je, wote hawaendi sehemu moja?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.