Mhubiri 5:3
Ecclesiastes 5:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama vile ndoto huja wakati kuna shughuli nyingi, ndivyo yalivyo mazungumzo ya mpumbavu wakati kuna maneno mengi.
Ecclesiastes 5:3 in English
Ecclesiastes 5:3 · Berean Standard Bible
As a dream comes through many cares, so the speech of a fool comes with many words.
Context
1Linda hatua zako uendapo katika nyumba ya Mungu. Karibia usikilize kuliko kutoa dhabihu ya wapumbavu, ambao hawajui kuwa wanafanya kosa. 2Usiwe mwepesi kuzungumza,
usiwe na haraka katika moyo wako
kuzungumza lolote mbele za Mungu.
Mungu yuko mbinguni
nawe uko duniani,
kwa hiyo maneno yako
na yawe machache. 3Kama vile ndoto huja
wakati kuna shughuli nyingi,
ndivyo yalivyo mazungumzo ya mpumbavu
wakati kuna maneno mengi. 4Wakati unapomwekea Mungu nadhiri, usikawie kuitimiza. Yeye hafurahii wapumbavu; timiza nadhiri yako. 5Ni afadhali usiweke nadhiri kuliko kuiweka na usiitimize.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.