Mhubiri 5:1
Ecclesiastes 5:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Linda hatua zako uendapo katika nyumba ya Mungu. Karibia usikilize kuliko kutoa dhabihu ya wapumbavu, ambao hawajui kuwa wanafanya kosa.
Ecclesiastes 5:1 in English
Ecclesiastes 5:1 · Berean Standard Bible
Guard your steps when you go to the house of God. Draw near to listen rather than to offer the sacrifice of fools, who do not know that they do wrong.
Context
1Linda hatua zako uendapo katika nyumba ya Mungu. Karibia usikilize kuliko kutoa dhabihu ya wapumbavu, ambao hawajui kuwa wanafanya kosa. 2Usiwe mwepesi kuzungumza,
usiwe na haraka katika moyo wako
kuzungumza lolote mbele za Mungu.
Mungu yuko mbinguni
nawe uko duniani,
kwa hiyo maneno yako
na yawe machache. 3Kama vile ndoto huja
wakati kuna shughuli nyingi,
ndivyo yalivyo mazungumzo ya mpumbavu
wakati kuna maneno mengi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.