Mhubiri 4:10
Ecclesiastes 4:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama mmoja akianguka, mwenzake atamwinua. Lakini ni jambo la kuhuzunisha kwa mtu yule aangukaye naye hana wa kumwinua!
Ecclesiastes 4:10 in English
Ecclesiastes 4:10 · Berean Standard Bible
For if one falls down, his companion can lift him up; but pity the one who falls without another to help him up!
Context
8Kulikuwepo mwanadamu aliye peke yake,
hakuwa na mwana wala ndugu.
Hapakuwa na mwisho wa kazi yake,
hata hivyo macho yake
hayakutosheka na utajiri wake.
Aliuliza, “Ninajitaabisha hivi kwa ajili ya nani,
nami kwa nini ninajinyima kufurahia?”
Hili pia ni ubatili,
ni shughuli yenye taabu! 9Wawili ni afadhali kuliko mmoja,
kwa sababu wana malipo mazuri kwa kazi yao: 10Kama mmoja akianguka,
mwenzake atamwinua.
Lakini ni jambo la kuhuzunisha
kwa mtu yule aangukaye
naye hana wa kumwinua! 11Pia, kama wawili wakilala pamoja
watapashana joto.
Lakini ni vipi mtu aweza
kujipasha joto mwenyewe? 12Ingawa mtu mmoja aweza kushindwa,
watu wawili wanaweza
kumkabili adui na kumshinda.
Kamba ya nyuzi tatu
haikatiki kwa urahisi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.