Kumbukumbu 9:22
Deuteronomy 9:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pia mlimkasirisha Bwana huko Tabera, Masa na Kibroth-Hataava.
Deuteronomy 9:22 in English
Deuteronomy 9:22 · Berean Standard Bible
You continued to provoke the LORD at Taberah,* at Massah,* and at Kibroth-hattaavah.*
Context
20Bali yeye alimkasirikia Aroni kiasi cha kutaka kumwangamiza, nami wakati huo nilimwombea Aroni pia. 21Kisha nikachukua ile sanamu ya ndama mliyoitengeneza na kuichoma kwenye moto. Nikaiponda na kuisaga ikawa unga laini kama vumbi, nikatupa lile vumbi kwenye kijito kilichotiririka toka mlimani. 22Pia mlimkasirisha Bwana huko Tabera, Masa na Kibroth-Hataava. 23Vilevile wakati Bwana alipowatuma kutoka Kadesh-Barnea, alisema, “Kweeni, mkaimiliki nchi ambayo nimewapa.” Lakini mliasi dhidi ya agizo la Bwana Mungu wenu. Hamkumtegemea wala kumtii. 24Mmekuwa waasi dhidi ya Bwana tangu nilipowajua ninyi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.