Kumbukumbu 9:13
Deuteronomy 9:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye Bwana akaniambia, “Nimewaona watu hawa nao ni watu wenye shingo ngumu sana!
Deuteronomy 9:13 in English
Deuteronomy 9:13 · Berean Standard Bible
The LORD also said to me, “I have seen this people, and they are indeed a stiff-necked people.
Context
11Mwisho wa siku arobaini usiku na mchana, Bwana alinipa mbao mbili za mawe, mbao za Agano. 12Kisha Bwana akaniambia, “Shuka chini mara moja, kwa sababu watu wako ambao umewatoa katika nchi ya Misri wamepotoka. Wamegeukia mbali haraka kutoka lile nililowaagiza, wamejitengenezea sanamu ya kusubu.” 13Naye Bwana akaniambia, “Nimewaona watu hawa nao ni watu wenye shingo ngumu sana! 14Niache, ili nipate kuwaangamiza na kufuta jina lao kutoka chini ya mbingu. Nami nitakufanya kuwa taifa lenye nguvu zaidi na kuwa wengi kuliko wao.” 15Kwa hiyo niligeuka na kuteremka kutoka mlimani kwani mlima ulikuwa ukiwaka moto. Pia vibao vile viwili vya Agano vilikuwa mikononi mwangu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.