Native Bible

Deuteronomy 7:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo, kuweni waangalifu kufuata maagizo, amri na sheria ninazowapa leo.

Deuteronomy 7:11 in English

Deuteronomy 7:11 · Berean Standard Bible

So keep the commandments and statutes and ordinances that I am giving you to follow this day.

Context

9Basi ujue kwamba Bwana Mungu wako ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayetunza Agano la upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaompenda na kuzishika amri zake. 10Lakini kwa wale wanaomchukia atawalipiza kwenye nyuso zao kwa maangamizi; hatachelewa kuwalipiza kwenye nyuso zao wale wamchukiao. 11Kwa hiyo, kuweni waangalifu kufuata maagizo, amri na sheria ninazowapa leo. 12Kama mkizingatia sheria hizi na kuzifuata kwa uangalifu, basi Bwana Mungu wenu atatunza Agano lake la upendo nanyi, kama alivyowaapia baba zenu. 13Atawapenda ninyi na kuwabariki na kuongeza idadi yenu. Atabariki uzao wa tumbo lenu, mazao ya nchi yenu, nafaka, divai mpya na mafuta, ndama za ngʼombe wa makundi yenu, na kondoo za makundi yenu katika nchi ile aliyoapa kuwapa baba zenu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.