Kumbukumbu 7:10
Deuteronomy 7:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini kwa wale wanaomchukia atawalipiza kwenye nyuso zao kwa maangamizi; hatachelewa kuwalipiza kwenye nyuso zao wale wamchukiao.
Deuteronomy 7:10 in English
Deuteronomy 7:10 · Berean Standard Bible
But those who hate Him He repays to their faces with destruction; He will not hesitate to repay to his face the one who hates Him.
Context
8Lakini ni kwa sababu Bwana aliwapenda ninyi na kutunza kiapo alichowaapia babu zenu kwamba atawatoa ninyi kwa mkono wenye nguvu na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa, kutoka nguvu za Farao mfalme wa Misri. 9Basi ujue kwamba Bwana Mungu wako ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayetunza Agano la upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaompenda na kuzishika amri zake. 10Lakini
kwa wale wanaomchukia
atawalipiza kwenye nyuso zao
kwa maangamizi;
hatachelewa kuwalipiza kwenye nyuso zao
wale wamchukiao. 11Kwa hiyo, kuweni waangalifu kufuata maagizo, amri na sheria ninazowapa leo. 12Kama mkizingatia sheria hizi na kuzifuata kwa uangalifu, basi Bwana Mungu wenu atatunza Agano lake la upendo nanyi, kama alivyowaapia baba zenu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.