Kumbukumbu 33:25
Deuteronomy 33:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Makomeo ya malango yako yawe chuma na shaba, nazo nguvu zako zitakuwa sawa na siku zako.
Deuteronomy 33:25 in English
Deuteronomy 33:25 · Berean Standard Bible
May the bolts of your gate be iron and bronze, and may your strength match your days.”
Context
23Kuhusu Naftali akasema:
“Naftali amejaa tele upendeleo wa Bwana,
naye amejaa baraka yake;
atarithi magharibi na kusini.” 24Kuhusu Asheri akasema:
“Aliyebarikiwa zaidi sana katika wana ni Asheri;
yeye na apate upendeleo kwa ndugu zake,
yeye na anawe miguu yake kwenye mafuta. 25Makomeo ya malango yako yawe chuma na shaba,
nazo nguvu zako zitakuwa sawa na siku zako. 26“Hakuna mwingine kama Mungu wa Yeshuruni,
ambaye hupanda juu ya mbingu ili akusaidie,
na juu ya mawingu katika utukufu wake. 27Mungu wa milele ni kimbilio lako,
na chini kuna mikono ya milele.
Atamfukuza adui yako mbele yako,
akisema, ‘Mwangamize yeye!’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.