Native Bible

Deuteronomy 33:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kuhusu Naftali akasema: “Naftali amejaa tele upendeleo wa Bwana, naye amejaa baraka yake; atarithi magharibi na kusini.”

Deuteronomy 33:23 in English

Deuteronomy 33:23 · Berean Standard Bible

Concerning Naphtali he said: “Naphtali is abounding with favor, full of the blessing of the LORD; he shall take possession of the sea * and the south.”

Context

21Alijichagulia nchi nzuri kuliko zote kwa ajili yake mwenyewe; fungu la kiongozi lilikuwa limehifadhiwa kwa ajili yake. Viongozi wa watu walipokusanyika, alitimiza haki ya mapenzi ya Bwana, na hukumu zake kuhusu Israeli.” 22Kuhusu Dani akasema: “Dani ni mwana simba, akiruka kutoka Bashani.” 23Kuhusu Naftali akasema: “Naftali amejaa tele upendeleo wa Bwana, naye amejaa baraka yake; atarithi magharibi na kusini.” 24Kuhusu Asheri akasema: “Aliyebarikiwa zaidi sana katika wana ni Asheri; yeye na apate upendeleo kwa ndugu zake, yeye na anawe miguu yake kwenye mafuta. 25Makomeo ya malango yako yawe chuma na shaba, nazo nguvu zako zitakuwa sawa na siku zako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.